Monday, 6 November 2017

KUJIFUNZA KWA KUTUMIA IMPRESS

Kwanini nijifunze kutumia Impress?
Impress ni njia maridhawa ya uwasilishaji mada inayowezesha utumiaji wa media mbalimbali. Mawasilisho ni njia inayotumiwa na walimu duniani kote katika kuwasilisha masomo kwa ufanisi na kwa ushirikishi. wanafunzi hufurahia matumizi ya tekinolojia na huonesha uelewa mkubwa pale mada inapowasilishwa katika njia tofauti na kuvutia. Impress inawapatia waalimu njia tofauti tofauti za kuwasilisha taarifa zao na kwa jinsi upatavyo ujuzi ndivyo uwezokano wa kuwa mjuzi zaidi pia
Uwasilisho wa Impress wa ni njia bora ya ufundishaji inayokuwezesha:
  • kujumuisha picha na michoro
  • kucheza video na rekodi
  • kutumia majedwali na grafu
  • kuunganisha maudhui yako na tovuti muhimu
  • kuwashirikisha wanafunzi wako kwenye ujifunzaji 
  • kuitumia kwa urahisi

No comments:

Post a Comment