Shule ya Msingi Mwenge yafanya Sherehe ya kuwaaga wahitimu wa Darasa la saba.Sherehe hii ya kuwaaga Darasa la saba mwaka 2022 ni sherehe ya kihistoria kwani ni sherehe ya 80.
Katika sherehe hii ya kihistoria vipaji mbali mbali vilionyeshwa na wanafunzi wahimu na wanaobaki.
Mgen rasm aliwaasa Wahitimu kuwasaidia wazazi kazi za nyumbani.Pia mgeni Rasmi ameahidi kuwapatia vifaa vya michezo wanafunzi wote walioshiriki michezo kwa ngazi ya mkoa hadi taifa.Mgeni Rasmi Pia ameahid kutengeneza uwanja wa Mpira wa net ball na kutoa zawadi ya mipira kwa shule
Mgeni Rasmi pia ameahidi mifunko 10 ya Sementi kwaajili ya Ujenzi wa Vyoo vya walimu na alitoa hamasa kubwa kwaajili ya kuanza harambee ya ujenzi wa Uzio wa shule hii ili wanafunzi waweze kuwa salama.

















