Saturday, 30 October 2021

Matokeo Darasa la Saba 2021 haya hapa, ufaulu waongezeka

 Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi 2021 na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.89.Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 907,802 waliofanya mtihani huo wamefaulu.Watahiniwa hawa wamepata alama 121 au zaidi kati ya alama 300” amesema.Amesema kati ya hao wasichana ni 467,967 (asilimia 81.43) na wavulana ni 439,835 (82.56).

No comments:

Post a Comment