Saturday, 30 October 2021

MATOKEO YA KUHITIMU DARASA LA SABA SHULE YA MWENGE YAZIDI KUFANYA VIZURI ZAIDI.

 Baada ya Matokeo ya darasa la Saba Mwaka 2021 kutangazwa  Shule yetu imezidi kufanya vizuri zaidi kwani imeshika nafasi ya 7 katika Manispaa ya Tabora na Kimkoa imekuwa nafasi ya 12.Kutokana na juhudi kubwa waliyofanya walimu hakuna Mwanafunzi mwenye Wastani wa D na E,Wote wana wastani wa A,B&C.

SOMA ZAID:-    Angalia hapa Matokeo ya Shule ya Mwenge.

Matokeo Darasa la Saba 2021 haya hapa, ufaulu waongezeka

 Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi 2021 na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.89.Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 907,802 waliofanya mtihani huo wamefaulu.Watahiniwa hawa wamepata alama 121 au zaidi kati ya alama 300” amesema.Amesema kati ya hao wasichana ni 467,967 (asilimia 81.43) na wavulana ni 439,835 (82.56).